Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

AY ampa tano Jaguar, kisa?

Msanii wa hip hip Bongo, AY amempongeza msanii mwenzie kutoka nchini Kenya, Jaguar kwa kuchaguliwa kuwa mbunge katika jimbo la Starehe.

Rapper huyo amesema ushindi wa Jaguar ameupokea kwa furaha kubwa kwa sababu anamfahamu zaidi na isitoshe alimtambulisha katika game ya muziki  rasmi pale walipotoa ngoma ya Nimetoka Mbali.

“Siku ambayo alisema anataka kuingia kwenye siasa nilishtuka kidogo lakini vitu ambavyo alikuwa anavifanya ni kama wanasiasa kabisa na pengine hata zaidi, so naamini jimbo la Starehe wamepata mtu sahihi na nina uhakika atawafanyia mambo makubwa,” AY amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times Fm na kuongeza.

“Kwa upande mwingine inaonyesha ukiwa na nia na kitu na ukakifanyia kazi utatimiza ndoto zako na utafanikiwa ndio kitu nimejifunza, pia inaonyesha mtu unaweza ukafanya muziki na jamii ikakukubali kwa upande mwingine, ukiona mifano kama wakina Mr Two, Professor Jay, Bobi Wine,” amesema.

AY ameendelea kusema ameongea na Jaguar na kumtakia kila la kheri na kumueleza amtangulize Mungu mbele katika kazi yake na vitu alivyoaidi azidi kutekeleza katika jamii.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW