DStv Inogilee!

AY hulipwa kila wimbo wake unaposikika Big Brother


Kuna faida nyingi mno za msanii anapotambulika kimataifa ambapo moja kubwa ni show nyingi za nguvu zinazomwijia kila kukicha.

AY aliligundua hilo mapema ndo maana hakuwa bahili kusafiri nje ya nchi kufanya collabo na wasanii wa kimataifa na kuingia gharama kubwa kufanya video.

Juzi tu ametoka Johannesburg kufanya video iliyochomoa zaidi ya milioni 31 kutoka kwenye akaunti yake.

Hivyo usishangae kuambiwa kuwa kila usikiapo wimbo wake umechezwa Big Brother Africa, kuna hela inaingia kwenye akaunti yake bila matatizo.

Jana wimbo wake Leo aliofanya na Prezzo ambaye ni mshikaji wake wa karibu, ulikuwa ukipigwa, na rais huyo wa Cash Money Brothers wa Kenya alikuwa akiiufurahia.

Lakini kuna mtu ambaye alitaka kujua zaidi kama AY anapata chochote kwakuwa hiyo si mara ya kwanza wimbo wake kuchezwa, “hivi kuna hela unalipwa kwa nyimbo zako kupigwa @BigBroAfrica?” ambapo AY alijibu “Yes baus.”

Kwa Bongo hiki ni kitu kigeni kwakuwa bado kuna mjadala mkubwa kati ya wamiliki wa radio na TV kuhusu kuwalipa wasanii kila wanapocheza nyimbo zao (radio/TV royalties) lakini kwa wenzetu hii ni njia mojawapo inayowaingiza pesa wanamuziki.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW