Burudani

AY husafiri popote na Biblia aliyoachiwa na marehemu mama yake


No wonder this dude is rich! Hatujawahi kuona msanii smart katika mambo yake kama Ambwene Yesaya, kuanzia katika kujiwekea ratiba ya wiki nzima kumwonesha nini anatakiwa kufanya wapi na nani, mpaka kusafiri na biblia ile ile aliyoachiwa na marehemu mama yake.
Juzi July 5, ilikuwa birthday yake ambapo kituo cha East Africa Radio kilimtembelea na kumfanyia mahojiano ya dakika tano tu lakini yaliyotoa vitu vipya kabisa ambavyo tulikuwa hatuvifahamu.
Mzee wa commercial ambaye wakati anaongea alikuwa anasound kama alikuwa ashapiga chupa mbili tatu za kuchangamsha akili yake, alisema mama yake aliwamwachia biblia ambayo tangu akabidhiwe mkononi hajawahi kuicha.
Kila unampomsikia amesafiri kwenda mikoani ama nchi za nje kupiga show ama shughuli binafsi, basi biblia hiyo lazima iwemo kwenye begi lake. Anasema hawezi kulala bila kusoma mistari kadhaa ya kwenye biblia hiyo hata kama akiwa amepiga mtungi kidogo.
“Tulipokuwa Mwanza juzi, Fid Q mwenyewe alinishangaa kuniona nasoma biblia” alisema.
Katika maongezi yake mama yake amemtaja sana. Aliongeza kuwa kila siku ya kumbukumbu ya kifo cha mama yake hufanya misa maalum kanisani na hajawahi kuacha kufanya hivyo.
Alitoa mfano kuna wakati siku hiyo ilimkuta Moscow, Urusi,ilibidi waaandaji wa show wafanye juu chini kutafuta kanisa kwaajili ya yeye kufanya misa hiyo na kupewa msaada na balozi wa Urusi.
“Heshimu wazazi wako upate miaka mingi ya kuishi duniani” biblia inasema hivyo right? na definitely kwa mfano wa AY tunaweza kusema, “Waheshimu,wapende ama wakumbuke wazazi wako muda wote ili upate mafanikio na pesa zaidi duniani”, lesson learned.
Now you know why AY receives continuous blessings in his career!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents