Burudani

AY kumtambulisha msanii atakayekuwa chini yake Jumapili hii

AY, Mwana FA na washkaji kwenye Fiesta Dar

Rapper/muimbaji na hitmaker wa Party Zone, Ambwene Yesaya aka AY amesema Jumapili hii kwenye ukumbi wa Billcanas atamtambulisha rasmi msanii wa kike ambaye atakuwa chini ya kampuni yake ya Unity Entertainment.

Akiongea na XXL ya Clouds FM leo, AY amesema pamoja na msanii huyo wa kike, atakuwa na msanii mwingine wa kiume ambaye atamtaja siku za usoni.

Ameongeza kuwa kampuni yake imewekeza hela nyingi kwa wasanii hao kwaajili ya kufanya video na audio za kimataifa kwakuwa kwa sasa anafanya kazi kiprofesheno zaidi.

Ili kuwatangaza, AY amesema atakuwa akitembea na wasanii hao kwenye show zake atakazokuwa akifanya sehemu mbalimbali.

Jumapili hii yeye na Cpwaa watakuwa na show waliyoipa jina la Road2CHOMVA2012 kwaajili ya kujiandaa na tuzo za Channel O za mwaka huu ambapo wote wanawania vipengele kadhaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents