Burudani

AY leo anashoot video ya Money nchini Afrika Kusini

Kama huelewi kwanini AY na washkaji zake wakiwemo Mwana FA na warembo Lamyia Good na Ms Triniti hujiita Team No Sleep, huenda sasa ukaanza kuelewa sababu.

Ni juzi tu usiku AY amejinyakulia tuzo ya video bora kutoka Afrika Mashariki kwenye tuzo kubwa za Channel O, na leo Jumatatu yupo location kushoot wimbo wake mpya Money aliomshirikisha Vanessa Mdee.

Hata hivyo huenda Vanessa asionekane kwenye video hiyo kwakuwa tweets zake za hivi karibuni zinaonesha kuwa mrembo huyo yupo jijini New York Marekani.

Hakijaharibika kitu hata hivyo kwakuwa, AY amechukua watoto wakali wa kuonekana kwenye video yake hiyo mpya kutoka kwenye kampuni iitwayo Clasiq Models ambayo huajiri wasichana wanaotumiwa kwenye video za wasanii.

Baadhi ya wasichana wa Clasiq Models

“At the the Sands shooting with @AyTanzania. Our girls look GOOD,” wametweet Clasiq Models.

Big ups kwa Team No Sleep ya Ambwene.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents