Burudani

AY na Cpwaa wapagawisha Billicanas Jumapili hii

Ay na Cpwaa wakihitimisha shoo ya kuelekea tuzo za Video za Muziki Za Channel O (CHOMVA 12)

Jana usiku katika kiota cha club ya usiku, Billicanas AY pamoja na Cpwaa walifanya shoo ya Road to Channel O Music Video Awards(CHOMVA) katika ile spesho sunday night “Usiku Wa club” ambao uliandaliwa mahsusi na kama sehemu ya kuwakumbusha watanzania kuwapigia kura wasanii hao wawili wanaowania tuzo za Channel O za mwaka huu zinazotarajiwa kufanyika nchini Africa Kusini katikati ya mwezi ujao na pia kutoa burudani kwa wapenzi wa wasanii hao ambao hawajawaona kwa muda mrefu.

Shoo hiyo ambayo iliandaliwa na SK Entertainemnt, Unity Entertainment, Club billicanas, TBC na Cpwaa ilihudhuriwa na mastaa wengine kibao walitokelezea kutoa sapoti kwa wasanii waliongozwa na produsa maarufu wa Mj Records Marco Chali, Ommy Dimpoz, mtangazaji Vanessa Mdee, Chidi Benz na wengine wengi ambao utawaona kwenye picha.

Shoo hiyo ilianza rasmi majira ya saa nane na ushee usiku ambapo Cpwaa aliingia stejini na kufuatiwa na madensa wake na kutumbuiza nyimbo mchanganyiko ambazo zimewahi kutamba tangu alipoanza muziki na pia kutumia fursa hiyo kuwakumbusha wapenzi wake kumpigia kura katika kipengele anachowania cha “Most Gifted Dance Video Of The Year” kabla ya kumkaribisha Mwana FA stejini ambaye naye hakuwaangusha wapenzi wa muziki waliofurika kwa wingi katika ukumbi huo ambapo na yeye aliimba nyimbo zake nyingi mchanganyiko.

Kama ilivyokuwa kwa Cpwaa MwanaFA aliwahamasisha wapenzi wa muziki wa Bongo Hip Hop na Bongo Flava, kuwa wawapigie kura wasanii hao kwani yeyote kati yao atakayeondoka na tuzo atakuwa anawawakilisha watanzania.

Kabla FA hajashuka aliamua kuchukua fursa hiyo kumleta Swahiba wake AY kwenye steji na kuimba wote takribani nyimbo mbili kabla ya AY kuendelea na makamuzi ya nguvu yaliyodumu kama nusu saa kwa kupiga nyimbo zake za zamani na za sasa kabla ya kuchukua fursa ya kumtambulisha msanii wa kike ambaye AY aliutangazia umma kati kati ya wiki iliyopita kwamba angemtambulisha siku ya jana katika shoo hiyo.

Msanii huyo ni Fezza Kessy aliyewahi kuwa mlimbwende wa Miss Tanzania katika miaka ya nyuma na kuamsha shangwe pale Fezza alipoimba kibao cha “Speak With ya Body”. Shoo iliendelea ambapo AY kama alivyotangulia Cpwaa aliwaomba wapenzi wa muziki wake kumpigia kura katika vipengele vitatu anazoziwania.

Vipengele wanavyowania AY na Cpwaa ni hizi zifuatazo:

AY:-
Most Gifted East African Video of the Year. Kumpigia kura katika kipengele hiki andika katika sehemu yako ya sms 13C, kwenda +27839208406
Most Gifted Male Video of the Year. Kumpigia kura katika kipengele hiki andika katika sehemu yako ya sms 1E, kwenda +27839208406
Most Gifted Video of the Year. Kumpigia kura katika kipengele hiki andika katika sehemu yako ya sms 14J, kwenda +27839208406

Cpwaa:-
Most Gifted Dance Video of the Year. Kumpigia kura katika kipengele hiki andika katika sehemu yako ya sms 5F, kwenda
+27839208406

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents