Burudani

AY na Fid Q wapeana mashavu kwenye mdundo wa Q the Don

Fid Q na AY wana historia nzuri ya kufanya hit pamoja. Kama unakumbuka AY alishawahi kumpa shavu la kuweka outro kwenye hit yake Usijaribu lakini pia Fid alimpa shavu hitmaker huyo wa Partyzone kwenye Shimo Limetema na Jeshi la Mtu Mmoja.

Screenshot - 4_30_2013 , 5_18_01 AM

Na sasa mastaa hao ambao majina yao halisi ni Ambwene Yesaya na Fareed Kubanda watasikika ngoma ngoma mpya, Jipe Shavu.

Wimbo huo ambao AY amemshirikisha Fid, umetayarishwa na producer Q The Don anayefahamika kwa hits kibao alizowahi kufanya kama Bang na Mchizi Wangu za Nako 2 Nako, CNN ya Ngwair na zingine.

Jipe Shavu itaachiwa Ijumaa hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents