Michezo

Azam FC haikamatiki Ligi Kuu ya Vodacom

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ‘VPL’ baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC ya mkoani Iringa bao 1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo Azam FC imefanikiwa kuifikia klabu ya Mtibwa Sugar kileleni baada ya kufikisha jumla ya pointi 10 huku ikiwa timu pekee ambayo haijaruhusu bao lolote tokea ligi hiyo ilipoanza Agosti 26 mwaka huu.

Kijana aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph ndiye aliyekuwa shujaa katika mchezo huo baada ya kuipatia Azam FC bao pekee dakika ya 11 akipokea pasi safi ya nahodha Himid Mao ‘Ninja’, likiwa ni bao lake la pili kwenye mechi ya pili mfululizo lingine akiitungua timu yake ya zamani Kagera Sugar katika ushindi wa 1-0.

Licha ya kufunga bao hilo, Azam FC ilifanikiwa kutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kutengeneza nafasi nyingi takribani 10 ambazo hazikutumiwa vema.

Lakini safu ya ushambuliaji ilikuwa ikiundwa na wachezaji vijana Yahya Zayd na Yusuph, ambao wanaendelea kujifunza mikikimikiki ya ligi hiyo,

Kabla ya mchezo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’, Wallace Karia, alipata fursa ya kuwakabizi tuzo za wachezaji bora wa Azam FC mwezi Agosti, beki, Yakubu Mohammed, akitwaa kwa upande wa timu kubwa na kiungo Twaha Ahmed, akibeba ya timu ndogo ‘Azam B’.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika kesho Jumatatu kanla ya kuanza mazoezi Jumanne kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Singida United, uutakaofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma Septemba 30 mwaka huu.

Kikosi cha Azam FC leo

Razak Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Agrey Moris, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Stephan Kingue/Braison Raphael dk 59, Frank Domayo, Salum Abubakar, Yahya Zayd/Wazir Junior dk 59, Mbaraka Yusuph/Yahaya Mohammed dk 79.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents