Michezo

Azam FC mambo ni moto michuano ya ASFC

Kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kimefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya Shupavu mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) uliyopigwa Mkoani Morogoro.

Waliyokuwa mashujaa katika mchezo huo ni Azam FC ni  Yahya Zayd aliyeanza kuiandikia bao la kwanza timu hiyo, Idd Kipwagile na Paul Peter aliyehitimisha karamu ya magoli kwa kupiga hat trick.

Azam FC imeingia kwenye mchezo huo dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL) ikiwa na kumbukumbu ya kuitoa Area C United ya Dodoma kwa mabao 4-0, yaliyofungwa na kiungo Salmin Hoza, Nahodha Msaidizi Agrey Moris, Yahya Zayd na Enock Atta.

Michuano hiyo ya Azam Sports Federation Cup ina umuhimu mkubwa kwa kila timu inayoshiriki kwakuwa mshindi huiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents