Michezo

Azam FC tuko vizuri – Himid Mao (Video)

Baada ya kurejea nchini jana jioni klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, ikitokea Uganda ilipokuwa imeweka kambi ya siku 10 kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nahodha wa timu hiyo, Himid Mao ‘Ninja’ amesema safari yao imekuwa na mafanikio makubwa kwakutimiza kile ambacho Kocha ameagiza kufanyika.

Nahodha wa Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’ 

Himid Mao ambaye pia ni nahodha msaidizi wa kikosi cha Stars amesema “Uganda hatukwenda kujifunza kitu bali kwenda kujiandaa na safari imekuwa na mafanikio makubwa kwakuwa tumekwenda kufanya kile ambacho mwalimu ametuagiza kufanya”, Mao ameyasema hayo wakati walipo wasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mao ameongeza kuwa “ Muunganiko upo mzuri tu licha yakuwa na wageni kwani wao ni wachezaji kwahiyo wamekuta wachezaji wengine na wanaungana kwa pamoja, kuondoka na kuingia wa wapya ni vitu vya kawaida hata ulaya hutokea kinachotakiwa ni wale waliyopo ni kuhakikisha wanaziba mapengo ya walo ondika”.

Azam FC imemaliza kambi hiyo kwa mafanikio makubwa ya kutopoteza mchezo hata mmoja baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers, huku ikitoka sare ya 2-2 na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ ya wachezaji wa ndani (CHAN), kisha ikakipiga na mabingwa wa nchi hiyo KCCA na kutoka sare ya 1-1.

Huku ikifanikiwa kuwachachafya wakusanyaji kodi wa Uganda timu ya URA kwa jumla ya mabao 2-0 kisha kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Onduparaka.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents