Michezo

Azam FC yakiri kumtambua Israel Nkongo kama mwamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga SC

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga dhidi ya Azam FC msemaji wa wana lamba lamba, Jaffary Idd amesema bado wanamtambua mwamuzi Israel Nkongo kuwa ndiyo msimamizi wa mchezo huo wa kesho na kumtaka kutenda haki kwenye mechi hiyo.

Azam FC hapo jana waliiandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakieleza kutokuwa na imani na mwamuzi huyo ambaye amepangwa kuchezesha mechi yao dhidi ya Yanga SC hapo kesho katika uwanja wa Chamazi Complex majira ya saa 10:00 jioni.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa Azam FC Idd Cheche amesema kuwa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu na kuwapatia raha mashabiki wake.

“Tumejiandaa kuhakikisha kuwa tunawapa raha na ladha ya soka mashabiki wa soka watakaojitokeza, hivyo tunawakaribisha na tunaiheshimu Yanga kama timu kubwa – Idd Cheche kocha msaidizi wa Azam FC.

Wakati hayo yakisemwa kwa upande wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu Yanga SC kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten amesema kilakitu kimekamilika kuelekea mchezo huo.

“Kila kitu kimekamilika kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam Fc,tunaiheshimu sana Azam kwani wamekuwa na msimu mzuri wanapata matokeo ndani na nje ya uwanja wao wa nyumbani ila ata sisi Yanga

SC tupo vizuri na tunatarajia kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho.”-Afisa habari Yanga SC Dismas Ten

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents