Michezo

Azam FC yatangaza mchezaji bora wa mwezi Agosti

Beki kisiki wa klabu bingwa ya Afrika Mashariki na kati Azam FC, Yakubu Mohammed, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa timu hiyo ijulikanayo kama (NMB Player Of The Month) mwezi Agosti mwaka huu.

Mohammed anayeunda safu ya ulinzi ya Azam FC ambayo ndio pekee mpaka sasa haijaruhusu wavu wake kuguswa tokea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ilivyoanza Agosti 26 mwaka huu, ametwaa tuzo baada ya kupendekezwa na kupigiwa kura nyingi na mashabiki wa soka kwenye mitandao ya kijamii ya timu hiyo.

Wachezaji wengine wa Azam FC wanaounda safu hiyo bora ya ulinzi ni beki, Agrey Moris, kipa Razak Abalora, Daniel Amoah na Bruce Kangwa huku wakishirikiana vema na safu imara ya kiungo chini ya Nahodha Himid Mao ‘Ninja’, Stephan Kingue, Frank Domayo na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Tuzo hiyo inayotolewa na mdhamini mkuu wa Azam FC (NMB) itatolewa leo Jumapili kabla ya kuanza kwa mchezo wa timu hiyo dhidi ya Lipuli ya Iringa saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents