Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Azam FC yatua kwakishindo Shinyanga

Kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kimewasili salama mkoani Shinyanga jioni ya leo tayari kuikabili Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ‘VPL’ unaotarajia kufanyika Jumamosi hii.

Azam FC imewasili ikiwa na kikosi kamili isipokuwa kiungo Stephan Kingue, ambaye bado hajapona vizuri majeraha ya mgongo, ambapo kabla ya kikosi hiko kuwasili hapo jana ilipumzika mkoani Dodoma na kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Gadafi.

Kikosi hicho kikiwa mkoani Shiyanga kimefikia katika Hoteli ya Vigimark, ambapo kwa mujibu wa programu ya kocha kesho ndio kitafanya mazoezi ya kwanza mkoani humo tayari kabisa kumalizia sehemu ya maandalizi ya kuwavaa Mwadui, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mwadui Complex.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW