Michezo

Azam FC yatua nchini kimya kimya (Picha)

Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imewasili nchini Jumanne jioni ikitokea nchini Uganda ilipokuwa imeweka kambi ya siku 10 na kufanikiwa kucheza michezo mitano ya kirafiki.

Kikosi cha timu ya Azam FC kikiwa kinawasili uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam

Azam FC imemaliza kambi hiyo kwa mafanikio makubwa ya kutopoteza mchezo hata mmoja baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers, huku ikitoka sare ya 2-2 na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ ya wachezaji wa ndani (CHAN), kisha ikakipiga na mabingwa wa nchi hiyo KCCA na kutoka sare ya 1-1.

Huku ikifanikiwa kuwachachafya wakusanyaji kodi wa Uganda timu ya URA kwa jumla ya mabao 2-0 kisha kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Onduparaka.

Ziara hiyo ya Azam inawaweka sawa kwaajili ya msimu ujao huku klabu hiyo ikitarajia kushiriki, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kombe la Mapinduzi na Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup.

 Zifuatazo ni picha zinazoonyesha matukio 

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents