Michezo

Azam FC yazikalisha Simba na Yanga kwenye historia ya Kombe la Mapinduzi

Klabu ya Azam FC jana usiku imefanikiwa kutetea kombe la Mapinduzi kwa kuifunga klabu ya URA kutoka Uganda kwa goli 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 za kawaida.

Ushindi huo wa jana wa Azam FC unakuwa ni ushindi wa nne tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 2007 ambapo imetwaa kombe hilo mwaka 2012, 2013, 2017 na 2018.

Klabu ya Azam FC kwa sasa inakuwa ndiyo klabu iliyochukua makombe mengi zaidi ikifuatiwa na Simba SC ambayo imechukua mara tatu huku klabu za Yanga SC, Miembeni FC, Mtibwa Sugar na KCCA zikitwaa kombe hilo mara moja.

Kwa rekodi nyingine ni kwamba Azam FC ndio klabu pekee iliyoweza kutetea ubingwa wake kwenye michuano hiyo awali hakukuwa na klabu iliyowahi kufanya hivyo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents