Uncategorized

Azania wafuata muongozo wa BoT kwa kufungua maduka 5 ya kubadilishia fedha za kigeni

Benki ya Azania (ABL) imefungua maduka matano maalum kwa ajiliya kubadirishia fedha za kigeni katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro ili kuwapa fursa wateja wa benki hiyo pamoja na wananchi wote njia rahisi ya kuweza kupata huduma hiyo muhimu katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.

Maduka ya kubadirishia fedha yaliyofunguliwa ni pamoja na katika Jengo la IPS na Hoteli ya
Seacliff jijini Dar es Salaam. Maduka mengine yamefunguliwa jijini Arusha, KIA pamoja na Moshi.

Huduma za kubadirishia fedha za kigeni zitakuwa zikitolewa kwenye maduka hayo kwa saa za
kawaida za kazi kama matawi mengine ya Benki ya Azania.

Uamuzi wa kufungua maduka haya mapya maalum kwa ajili ya huduma za kubadirishia fedha za
kigeni tu, unatokana na mwongozo wa hivi karibuni wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama hatua
ya kuhakikisha watoa huduma wote wa kubadiri fedha za kigeni wanatambuliwa na BoT.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa Benki ya Azania kufungua maduka hayo mapya, Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo, Charles J Itembe amesema benki inajivunia kupanua wigo wake hususani
katika kutoa huduma za kubadirisha fedha za kigeni katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika
maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi wa huduma hiyo.

“Licha ya kutoa huduma ya kubadiri fedha za kigeni, maduka haya mapya yatakuwa na uwezo wa
kutoa huduma nyingine za kibenki kama vile kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha pamoja
na huduma za kifedha kwenye simu za mkononi (sim banking)”. Amesema Itembe.

Itembe pia ameongeza kuwa Benki ya Azania itaendelea kuwa na madirisha ya kubadiri fedha za
kigeni kwenye matawi yake yote nchini mbayo huwa wazi kila siku kuanzia saa mbili asubuhi
mpaka saa mbili usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents