Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Baada ya ajali ya kugongana, hii ndio taarifa rasmi ya afya ya Okwi na Omog

Jana kocha wa klabu ya Simba, Joseph Omog na Mshambuliaji wa klabu hiyo, Emmanuel Okwi walipata ajali ya kugongana wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, habari nzuri ni kwamba wawili hao afya zao zinaendelea vizuri kwani leo wameonekana mazoezini.

Kikosi cha Simba kikiwa mazoezini

Meneja wa Simba, Cosmas Kapinga amethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa wawili hao wapo katika hali nzuri kiafya.

Taarifa za awali jana ziliripoti kuwa wawili hao baada ya kugongana walipelekwa hospitali kwa matibabu.

Klabu ya Simba ipo kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo wake wa Ligi kuu dhidi ya Mwadui FC, utakaochezwa Jumapili Septemba 17.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW