Baada ya Al ahly kutwaa ubingwa jana , hizi ndio timu 10 zilizoshinda mara nyingi taji hilo la CAF Champions league

Bao la dakika za mwisho la Mohamed Magdy liliipatia ushindi Al Ahly dhidi ya mahasimu wao wa Cairo Zamalek katika fainali ya ya klabu bingwa barani Afrika.

Bao la Magdy la dakika ya 88- ilikamilisha mechi ya kusisimua ambayo timu yake ilikuwa kifua mbele mapema kupitia goli la Amr El Soleya, lakini likasawazishwa kabla ya muda wa mapumziko.

Ahly ingelikuwa tayari inaongoza lakini Elshahat alishindwa kufunga bao la wazi katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili.

Ushindi huo uliwapatia rekodi ya kuendelea kushikilia taji hilo la klabu bingwa barani afrika kwa mara ya tisa, na kumanisha kuwa mkufunzi wao kutoka Afrika Kusini Pitso Mosimane, kuwa kocha wa tatu kushinda taji hilo na klabu mbili tofauti.

Mashambulizi ya ajabu

Shikabala aliposawazisha bao dhidi ya Al Ahly
Shikabala aliposawazisha bao dhidi ya Al Ahly

Mashindano ya mwaka 2020 yalicheleweshwa kutokana na janga la Covid-19, huku hatua zilizochukuliwa kudhibiti kuenea kwa virusi ikilazimu finali ya kwanza ya klabu bingwa Afrika kati ya timu mbili kutoka nchi moja kuchezwa bila kuwa na mashabiki uwanjani.

Unaweza kutafakari hali ingelikuwa ndani ya uwanja wa kimataifa wa Cairo ikiwa mashabiki wangeliruhusiwa uwanhani. Hata hivyo wale waliokuwa wakifuatilia mechi hiyo kutoka miji tofauti na nchi zingine barani Afrika- walitazama mchezo wa kusisimua ikizingatiwa taharuki inayokumbwa mashabiki kutokana na ushindani unaoshuhudiwa katika mechi kubwa kama hiyo.

Hali hiyo ilitulizwa kwa kiwango fulani baada ya Al Ahly kutangulia kufunga bao.

Walitumia nafasi yao vizuri kuanzia mwanzo, dakika nne baada ya mechi kuanza walipata kona ya kwanza kutokana na juhudi za winga wao matata Hussein Ali Elshahat.

Kutokana na kona hiyo, El Soleya alishambulia safu ya ulinzi ya Zamalek na kutia kimyani bao la nguvu.

Zamalek walitikiswa na bao hilo na iliwachukua muda kabla ya kurejea kwenye mchezo. Baada ya dakika 20 walianza kushambulia lango la Al Ahly.

Juhudi zao zilizaa matunda katika dakika 31, nahodha wao Shikabala, alifunga bao la kusisimua ambalo lisawazisha mechi hiyo katiak kipingi cha kwanza.

Al Ahly v Zamalek
Mchezo huo ulikabiliwa na ushindani mkali

Baada ya bao la Shikabala, mechi hiyo iliendelea kuchezwa kwa mwendo wa kasi huku kila upande uking’ang’ania kushambulia ngome ya mshindani hato kutoka nje ya sehemu ya penati hali ambayo iliongezea bondo mchezohuo.

Ahly, hata hivyo ilipoteza nafasi ya wazi katika dakika ya 53 – baada ya mchezaji Elshahat kushindwa kufunga bao baada ya kuwapita walinzi wote wa Zamalek na kipa Gabal Ali.

Pande zote mbili zilifanikiwa kutumia kasi ya mawinga wao- Zizo wa Zamalek na Magdy wa Ahly – kutafuta ushindi.

Lakini mchezo huo ulionekana kuelekea katika muda wa ziada baada ya Magdy kukabwa katika safu ya kushoto, mbali na lango Zamalek.

Hata hivyo alijikakamua na kupita eneo hilo, na kudhibiti mpira kwa kutumia goti, kuupiga juu na kuutuliza kabla ya kupiga kiki moja hatari na kumpita kipa Gabal Ali wa Zamalek.

Hatua hiyo ya Magdy ilikuwa ya kimataifa – na iliifanya wachezaji wa Ahly kushangilia kwa furaha wakifahamu kuwa wao ndio mabigwa wa Afrika.

Orodha ya timu (vilabu0 13 barani Afrika vilivyofanikiwa kushinda taji la klabu bingwa mara nyingi zaidi.

 

Performances in the African Cup of Champions Clubs and CAF Champions League by club
ClubTitlesRunners-upSeasons wonSeasons runner-up
Egypt Al Ahly941982198720012005200620082012201320201983200720172018
Egypt Zamalek5319841986199319962002199420162020
Democratic Republic of the Congo TP Mazembe521967196820092010201519691970
Tunisia ES Tunis4419942011201820191999200020102012
Guinea Hafia FC3219721975197719761978
Morocco Raja Casablanca311989199719992002
Cameroon Canon Yaoundé30197119781980
Ghana Asante Kotoko251970198319671971197319821993
Morocco Wydad Casablanca221992201720112019
Algeria JS Kabylie2019811990
Nigeria Enyimba2020032004
Algeria ES Sétif2019882014
Democratic Republic of the Congo Vita Club12197319812014

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW