Habari

Baada ya basi la wanafunzi kutekwa na kuteketezwa kwa moto wakielekea mazoezini, dereva atiwa mbarani akihusishwa na tukio hilo (+ Video)

Basi lililokuwa limebeba watoto wa shule wapatao 51 lilitekwa na dereva wake na kisha kutiwa moto karibu na Milan nchini Italia. Watoto hao wa shule, baadhi yao walifungwa kamba, waliokolewa baada ya kuvunjwa vioo vywa basi hilo upande wa nyuma na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya.Watu kumi na wanne waliathiriwa na moshi uliotokana na kuteketea kwa basi hilo.

Dereva wa basi hilo alikuwa na umri wa miaka arobaini na saba mwenye uraia wa nchini Italia ingawa ana asili ya kutoka nchini Senegal, inaarifiwa kwamba ametiwa nguvuni.

Kwa mujibu wa BBC. Dereva huyo alisikika akitamba, akiwaambia waliokuwemo katika basi hilo kwamba hakuna hata mtu mmoja atakaye nusurika.Ulikuwa ni muujiza, vinginevyo yangekuwa ni mauaji ya halaiki, alinukuliwa akisema hayo mwendesha mashtaa mkuu wa mjini Milan, Francesco Greco.

Mwalimu mmoja wapo alikuwa ndani ya basi wakati tukio hilo likitekelezwa, alimuelezea mtuhumiwa huyo kuwa alikuwa na silika ya hasira mara kwa mara na kubwa hasa ni juu ya sera za wahamiaji nchini Italia .Taarifa zingine zinaarifu kuwa dereva huyo alisikika akibwata sitisheni mauaji katika bahari ya Mediterranean”.

Tukio hilo lilikuwaje?

Makundi mawili ya wanafunzi waliokuwa wakisindikizwa na waalimu wao , walikuwa wameyatoka mazingira ya shuleni iitwayo Vailati di Crema , wakielekea kwenye mazoezi lakini baadaye gari ikachukua muelekeo tofauti na safari yao na kuelekezwa kwenye barabara kuu ya mkoa na kufuata njia inayoelekea katika uwanja wa ndege wa Milan Linate, ripoti za mashuhuda zinaarifu .

Suala hilo liling’amuliwa dakika arobaini baadaye , wakati dereva alipowaelekezea abiria wake kisu huku akizungumza, mvulana mmoja aliwapigia wazazi wake kwa siri, ambao nao waliwafahamisha polisi juu ya tukio hilo.

Ilichukua muda kidogo kabla polisi hawajalifikia basi lililotekwa na kujaribu kulifanya lisimame,na mara basi hilo lilianza kubamiza gari la polisi kabla ya kupunguza mwendo na kusimama kabisa.

Taarifa kutoka nchini Italia zinaarifu kuwa mafuta ya petroli yalinyunyizwa kulizunguuka basi hilo la shule , lakini polisi walitumia mbinu ya kuvunja mairisha ya nyuma ya basi hilo na hivyo kuwaruhusu abiria kushuka kwa haraka kabla basi hilo halijalipuka moto.

Waendesha mashitaka wa Milan waliarifu kuwa wanafanya uchunguzi wa kina kuchunguza ikiwa kulikuwa na nia zozote mbaya ikiwa ni pamoja na ugaidi.Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Salvini, alizungumza kwa hasira kwamba dereva huyo alikuwa na rekodi ya uhalifu.

Picha sio ya tukio husika

msimamo mkali wa Italia kwa wahamiaji

Tangu alipoingia madarakani mwezi wa sita mwaka jana, uongozi wa Italia wa chama cha mrengo kulia na harakati za umoja wa Wanawake wenye hadhi ya nyota tano wameanzisha harakati zenye msimamo mkali wa kupambana na uhamiaji nchini humo.

Harakati hizo zimepamba moto na kuwa za mstari wa mbele dhidi ya wahamiaji wanaovuka Bahari ya Mediteranean kwenda Ulaya, nayo Italia imejaribu kufunga bandari zake kwa kutumia boti.

Mapema wiki hii, watu karibu hamsini waliokolewa na meli ya wasamaria wema ambapo wahamiaji walikuwa wakisafiri kwenye boti iliyotengenezwa kwa plastiki ikielea katika pwani ya Libya na kuchukuliwa hadi katika pwani ya Sicilia ya Lampedusa.

Mamlaka nchini Italia iliamuru kukamatwa kwa meli hiyo na kuanzisha uchunguzi juu ya madai ya kuhamia uhamiaji wa siri.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents