Michezo

Baada ya Beckham, sasa Mamadou wa Liverpool ala bata nchini

Siku chache baada ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester united, David Beckham  kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutalii akiwa na familia yake.

             Mchezaji wa klabu ya Liverpool, Mamadou Sakho

Safari hii ni Mfaransa, Mamadou Sakho beki wa Liverpool tayari yupo nchini akila kuku kwa mrija  mkoani Arusha na kutazama namna Tanzania ilivyojaaliwa maliasili.

Taarifa zinaeleza Sakho yupo nchini akiwa ameongozana na mkewe Majda na wanatarajia kutembelea katika mbuga za wanyama ingawa imekuwa ikifanywa siri kubwa.

 Mchezaji wa klabu ya Liverpool, Mamadou Sakho akiwa na watanzania

Mchezaji huyu ambae kwa sasa anakipiga katika klabu ya Crystal Palace kwa mkopo, yuko mapumzikoni na amechagua kuja mbuga za wanyama za Tanzania .

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents