Michezo

Baada ya Everton, Daylan Kerr wa Gor Mahia aitamani Simba, Yanga

Kocha Mkuu wa klabu ya Gor Mahia, Daylan Kerr amekiri kufurahishwa na Uwanja wa Taifa wa Tanzania huku akidai yupo tayari kupokea mwaliko siku yoyote kwaajili ya timu yake hiyo kucheza na Simba au Yanga.

Daylan Kerr

Muingereza huyo ambaye timu yake wiki jana ilikubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Everton ya Uingereza, amesema Tanzania ina mazingira mazuri ya kisoka licha ya kuwa na changamoto ya kutofanya vizuri kimataifa.

“Uwanja ni mzuri sana, kama unacheza hapa ni kama upo Old Trafford, tungependa tena kurudi hapa kama tukialikwa,” Kerr aliiambia Bongo5. “Tukialikwa na Simba, Yanga hata Azam tutafurahi kwa sababu zote ni timu nzuri ambazo zinaweza kutufanya kuwa vizuri katika msimu wetu ujao wa ligi,”

Kocha huyo ambaye ni mgeni katika kikosi hicho cha Gor Mahia, aliwahi kuifundisha klabu ya Simba ya nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents