Burudani ya Michezo Live

Baada ya Forbes kumtoa Kylie Jenner kwenye orodha ya mabilionea, Wakidai utajiri wake ni wauongo uongo awajia juu

Moja ya habari kubwa siku ya leo ni kuwa Jarida la Forbes limemfuta Kylie Jenner kutoka kwenye orodha yake ya mabilionea wenye umri mdogo zaidi duniani na wakailaumu familia yake kwa kuwapotosha. . . “Familia yake ilifanya jitihada za kuwapotosha wakaguzi wetu ili kumuonesha binti huyo mdogo katika familia maarufu ya Kardashian kuwa ni bilionea kutokana na mauzo ya vipodozi’’.

Jenner aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hakuwashawishi Forbes kumtambua na kuwa anashangaa kwanini wanaandika habari zisizokuwa na ukweli wowote.
“Ninaweza kutaja vitu 100 ambavyo ni vyenye umuhimu zaidi maishani mwangu, jarida hili limeandika maneno ambayo si ya kweli.”


Mwezi Mach Jenner alitangazwa kuwa moja wa mabilionea wenye umri mdogo kwa mujibu wa orodha ya mabilionea ya gazeti la Forbes. Akiwa na umri wa miaka 21-Kylie alianzisha na anamiliki kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, biashara ya urembo ambayo imedumu kwa miaka mitatu sasa na kuingiza mapato ya takriban dola milioni $360m mwaka jana.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW