Burudani

Baada ya Hamisa kusema sio single Mother, awacharukia wanaombeza ‘kisa nimezaa na wanaume wenye hela’

Mwanamitindo, Hamisa Mobetto amewajiwa juu wanaomsema vibaya baada ya video yake ya jana kusambaa akifunguka juu ya maisha ya malezi ya watoto wake.

Katika video hiyo alisema yeye sio Single Mother kwani watoto wote wanahudumiwa na baba zao, Kupiti mtandao wa Snapchat Mrembo huyo aliandika “Alafu ngoja niwaambie kitu. Mimi ni mbaya kweli nakubali kabisa, alafu pia ni maskini kweli kwenye maisha bado najikongoja kwahiyo hayo sio matusi bali ni hali halisi. Kwahiyo mkikubali hali kama niliyokubali mie labda mtaacha matusi yasio na faida.”

Aliongeza kuwa “Alafu miaka inaenda siku zinakimbia pia…hamuwezi kuwa mna hasira kila siku kisa nimezaa na wanaume wenye hela..hivi nachanganyikiwa au? maana sababu ningine hamna zaidi ya hao wanaume wawili.”

Aliendelea kuandika hivi, “Mnatakiwa mjua kwamba Fancy na Dee Mungu ndo alipanga wazazi wa hawa watoto wawe nani..hasira zenu please msinimalizie mie mtoto wa marehemu Mzee hassan..Its getting boring now.”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents