Baada ya Huddah kumkana Colonel Mustapha sio mpenzi wake, wawili hao waendelea kujibishana mtandaoni

Zile drama za kwenye mitandao ya kijamii zimeingia katika hatua nyingine baina ya mastaa wawili wa Kenya rapper Colonel Mustapha na aliyekuwa mwakilishi wa BBA Huddah Monroe.

huddah
Baada ya wawili hao kugeukana siku chache baada ya kutangaza kuwa ni wapenzi kupitia Interview waliyofanya na KTN, Huddah na Mustapha bado hawajamalizana ambapo hivi sasa wameingia katika hatua nyingine ya kurushiana vijembe kupitia mitandao ya kijamii, kitu ambacho si kigeni kwa Huddah na wapenzi wake waliopita.

Baada ya kujiondoa Twitter bila kusema sababu, jana Huddah alilianzisha tena kwa kumpiga kijembe Mustapha kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa kumwambia kuwa hakuwa class ya wanaume anao date nao.

“Class ya wanaume ninao-date nao wako busy wakitafuta kuingia katika orodha ya Forbes sio busy kutafuta umaarufu wa mitandao ya kijamii” aliandika Huddah.
Aliendelea, “Never seen a man so bitter over a woman he only saw half naked a photo shoot….Chill, at least u got to take to floss with!.”

Kama ulivyo mchezo wa masumbwi unapopigwa konde nawe unajibu (kama bado unakuwa na nguvu hizo), Mustapha naye alimjibu.

“I have moved on, I suggest she does the same,Next time, she should be wise n not leave photographic evidence! Ati anadate jamaa class ya forbes? haahahahahaha akapige picha na Bill Gates!.”

Hata hivyo Huddah alifuta post hiyo muda mchache baadaye.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW