Burudani

Baada ya kifo chake Juice Wrld avunja rekodi ya kusikilizwa zaidi – Video

Baada ya kifo chake Juice Wrld avunja rekodi ya kusikilizwa zaidi - Video

Baada ya kifo cha ghafla cha Juice WRLD akiwa na umri wa miaka 21, huku kifo chake kikielezwa kusababishwa na Kifafa ambacho kilipelekea kuanza kutokwa na damu mdomoni.

OAKLAND, CA – SEPTEMBER 29: Rapper Juice Wrld performs at the 2019 Rolling Loud Music Festival on Day 2 at Oakland-Alameda County Coliseum on September 29, 2019 in Oakland, California. (Photo by Steve Jennings/FilmMagic)

Mashabiki wa rapper huyo katika jimbo la Chicago walianzisha kampeni ya kuusapoti muziki wake na kupelea muziki wa Juice kuvunja rekodi kwa kusikilizwa sana nchini Marekani.

Kwa kupitia mtandao wa Rolling Stone.muziki wake umesikilizwa zaidi kwenye mitandao na kumfanya kuwa msanii ambaye amesikilizwa zaidi (Most-Streamed Artist) kwa Marekani.

Disemba 8 ambayo ndio ilikuwa siku ya Kifo chake, muziki wake ulipanda zaidi kwa asilimia 487 ukisikilizwa zaidi ya mara milioni 38 kwa Marekani, ikiwa ni mara milioni 24 zaidi ya msanii yoyote kwa siku hiyo. Top 3 ya mitandao mikubwa duniani (Apple Music, Spotify na Amazon Music) ilitawaliwa na muziki wake.

Ngoma zake kama “Legends” na “Lucid Dreams” zimetajwa kuongoza kwenye Chart za mitandao hiyo na mauzo pia.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents