Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Baada ya kuchezea kichapo ulingoni hatimaye, David Haye atangaza kustaafu masumbwi

Mwanamasumbwi bingwa wa Dunia, David Haye ametangaza kustaa mchezo huo hii leo ikiwa imepita mwezi mmoja pekee tangu kupoteza pambano lake la marudiano dhidi ya Tony Bellew ndani ya ulingo.

Bondia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 37, ameamua kutangaza kuachana na ngumi baada ya mapambano yake 32 toka kuanza mchezo huo huku akishindwa kufua dafu mbele ya Bellew mwezi mmoja uliyopita.

Akiwa ameanza mapambano ya kulipwa mwaka 2002, Haye amefanikiwa kushinda michezo 28 huku akiwapiga watu kwa KO mara 26 na kupoteza minne pekee kwa muda wote huo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW