Burudani

Very soon! Alikiba kudondosha kolabo na kundi hili maarufu nchini Kenya

Baada ya kutisha na ngoma kali ya Unconditionaly Bae akiwa na kundi la Sauti Sol, Alikiba ameingia tena studio wikiendi hii nchini Kenya akiwa na kundi la H-Art The Band kuandaa mdundo mpya.

Alikiba akiwa studio

Vyanzo vyetu vimeeleza kuwa ngoma hiyo itakuwa ni ya Alikiba akiwa amewashirikisha H-Art The Band na tayari wiki hii wameshamaliza ku-shoot video ya wimbo huo.

Alikiba toka wiki iliyopita yupo nchini Kenya kwa kazi hiyo maalumu ya kuandaa ngoma hiyo na imeandaliwa na producer maarufu nchini Kenya, Cedo.

Kwa ufupi, Cedo ndiye producer aliyetengeneza hit songs kibao za Nyashinski ikiwemo “Mungu Pekee”, “Malaika”, na “Hayawani”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents