Burudani

Baada ya kukiri kufulia, Nay wa Mitego aja na jipya hili (+Video)

By  | 

Baada ya wiki iliyopita kutangaza kuwa ameuza magari yake yote na kwa sasa anatembelea daladala na bajaji. Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nay wa Mitego amekuja na tamasha lake aliloliita ‘Nguvu ya Kitaa’.

Nay wa Mitego amesema lengo la kuanzisha tamasha hilo ni kusaidia mashabiki wake wenye kipato kidogo, kushudia muziki mzuri kutoka kwake na wasanii wengine ambao watamsindikiza kwa bei nafuu.

SOMA ZAIDI – Nay wa Mitego akiri kuuza magari yake yote ‘kwa sasa napanda daladala’

Tamasha hilo litafanyika mikoa mitano na litajumuisha wasanii kibao wa Bongo Fleva akiwemo QBoy Msafi, Pam D, Chemical na wengineo kibao.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments