Burudani ya Michezo Live

Baada ya kumpiga mzungu KO ndani ya sekunde 43, Mbabe Deontay Wilder amtumia salamu za vitisho Antony Joshua

Alfajiri ya kuamkia Leo Mei 20, 2019 nchini Marekani kulikuwa na pambano la ngumi uzito wa juu kati ya Mbabe Deontay Wilder na Dominic Brazeale, Pambano ambalo Wilder ameibuka kwa ushindi wa KO ndani ya sekunde 44 za raundi ya kwanza.

Deontay Wilder

Baada ya ushindi huo Wilder akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa mchezo huo alihisi utakuwa rahisi ila sio kwa ushindi alioupata.

Alipoulizwa kuhusu nia yake ya kupambana na Antony Joshua kama bado ipo, Wilder amesema hao wrote pamoja Tyson Furry wapo kwenye mipango yake na atawapitia kama upepo.

“Hao wote wapo kwenye mipango yangu, nadhani yeye na Tyson watapitia kwenye mikono yangu kama nilivyofanya leo, Ni muda tu unasubiriwa,” Amesema Wilder.

Ushindi wa Jana wa Wilder unamfanya kufikisha KO 40 kati ya mechi 42 alizocheza kwa muda wote.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW