Habari

Baada ya kumtukana Mungu, Rais Duterte akataa kuwaomba radhi Wakristo ‘Mungu wenu simjui namjua Allah’

Baada ya kumuita Mwenyezi Mungu ‘Mpumbavu’ Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa hajatenda kosa lolote kwani anaamini Mungu wa Wakristo hususani anayeabudiwa na Waumini wa Kanisa la Katoliki sio Mungu wa kweli.

Image result for rodrigo duterte
Rais Rodrigo Duterte

Kwa mujibu wa gazeti la The Philippine STAR, umeleeza kuwa Duterte amesema hayo jana kwenye mkutano wa kutafuta suluhu juu ya kauli yake ya kumtukana Mungu na kulishambulia Kanisa Katoliki nchini humo.

Duterte amesema kuwa yeye kwa sasa sio Mkristo tena kwani amekosa imani na Biblia huku akieleza kuwa ataendelea kuamini kuna Mungu wa kweli ambaye siye huyo anayeabudiwa na Wakristo bali ni Allah.

SOMA ZAIDI – Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amkashfu Mungu na kuliponda Kanisa Katoliki ‘mpumbavu, alitegemea nini kuwaumba Adam na Eva’

Kauli za rais Duterte zinakinzana kila mwaka na ni kawaida yake kushambulia dini au madhehebu pale anapokuwa na kusudi lake.

Rais huyo aliyewahi kujiita kuwa yeye ndiye Rais bora Duniani amekaririwa na gazeti hilo akisema “sioni kosa langu hivyo ndivyo ninavyo amini Wakristo Mungu wenu mnamjua wenyewe mimi naamini Mungu wa kweli ni mmoja ‘Allah'”

Mwaka 2016 kabla ya kuingia madarakani alikaririwa akiwakandia Viongozi wa makanisa ya Katoliki kuwa ni watu wabaya wanaowaombea wauza madawa ya kulevya wamrudie Mungu ile hali wanaiharibu jamii.

Alikaririwa akisema anamuamini sana Allah kuliko Mungu wa Wakristo kwani anaruhusu watu waovu kuombewa badala ya kuadhibiwa vikali.

Hata hivyo, haikutosha mwaka huo huo miezi miwili baada ya kuingia madarakani alianza kuwashambulia waislamu kwa kuwaita magaidi hii ni baada ya kikundi chenye itikadi kali za kiislamu cha  Abu Sayyaf kuwaua wanajeshi 15 wa Ufilipino.

Mpaka sasa Rais Duterte amekataa kabisa kuitwa Mkristo lakini bado hajatangaza kuwa ni Muislamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents