Michezo

Baada ya kupoteza mbele ya Senegal ’Simba wa Teranga’ Hassan Kessy afunguka “Miaka mingi hatujacheza mashindano haya, tutafanya vizuri mchezo unaokuja“ (+Video) 

Nyota wa timu ya taifa ya Tanzania, Hassan Kessy amewashukuru Watanzania kwa mchango wao mkubwa waliouonyesha dhidi ya Senegal, huku akiwaomba radhi kwa matokeo mabovu waliyopata kwenye mchezo huo wajana usiku.

Kessy ambaye anacheza nafasi ya beki wa kulia wa Stars na klabu yake ya Nkana FC ameyaongea hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo waliyopoteza kwa mabao 2 – 0.

“Ni makosa madogo madogo ambayo tumeyafanya na wenzetu wakayatumia, tunapenda kuwashukuru Watanzania wote ila hii ndiyo changamoto ambayo tunakutananayo.“ – Amesema Kessy.

Hata hivyo beki huyo wa klabu ya Nkana FC ya nchini Zambia ameongeza “Miaka mingi sana hatujawahi kucheza mashindano haya kwahiyo tunapata changamoto kubwa sana, kikubwa huu ni mwanzo tunahakikisha tutafanya vizuri kwenye mchezo unaokuja mbeleni.“

aifa Stars ilikubali kipigo cha mabao 2 – 0 kutoka kwa Senegal katika mchezo wao wa kwanza wa kundi C ya michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri.

https://www.instagram.com/p/BzFXvWbhh0R/

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents