Burudani

Baada ya kutangaza kuacha muziki, Q Chief apigiwa simu na Mzee wa Upako

Baada ya kuweka wazi dhamira yake ya kuacha muziki, msanii Q Chief amesema amepigiwa simu na watu wengi mmoja wapo ni Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’

Muimbaji huyo amesema kuwa Mzee wa Mpako alionyesha kuguswa na hatua hiyo aliyoamua kuichukua.

“Nimepokea simu kutoka kwa mtu kama Anthony Lusekelo, usiku saa tisa unaweza kuona ni jinsi gani mchungaji anaweza kuguswa na kusema mwanangu nimetaka kama kulia hivi, nimepigia simu na maostadhi wakubwa sana Tanzania hii,” Q Chief ameiambia Clouds TV.

Ameongeza kuwa amefikia maamuzi hayo na hana kinyongo chochote na mtu ila kwa sasa ameona mapenzi makubwa sana kutoka kwa watu kwenda kwa Q Cheif.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents