Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Baada ya kuzikwa na mamilioni, Kaburi la aliyekuwa mume wa Zari ‘Ivan’ lafukuliwa

Kaburi la aliyekuwa mume wa Zari,  Ivan Ssemwanga limefukuliwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Nakaliro mjini Kayunga nchini Uganda.

Kaburi la Ivan lilivyofukuliwa na watu wasiojulikana (Picha na Fred Muzaale)

Ivan ambaye mwili wake ulizikwa kwa maburungutu ya fedha, kabuli lake limefukuliwa usiku wa kuamkia jumatano ya Desemba 6 mwaka huu ambapo mashuhuda wamesema watu hao walikuwa na lengo la kuchukua fedha ambazo alizikwa nazo.

Nilishtuka alfajiri baada ya kusikia mbwa wakibweka kwa sauti makaburini ndipo nilipotoka nikakuta kaburi likiwa na shimo kubwa ubavuni lakini sikujua watu hao ni akina nani.“amesema shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la  Wamala kwenye mahojiano yake na gazeti la Daily Monitor.

Milionea Ivan ambaye alikuwa ni mmiliki wa  ‘Rich Gang Crew’ majirani zake wanasema walisikia kelele za mbwa zikibweka alfajiri ya kuamkia jumatano.

Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda limeripoti kuwa familia ya Ivan iliajiri walinzi kulinda kaburi hilo kwa kuwalipa kiasi cha shilingi milioni 1 za Uganda kwa mwezi ambapo tangu afariki mwezi May walinzi hao wamelipwa kiasi cha shilingi laki 6 tu za Kiganda.

Ivan alifariki tarehe 25 May mwaka huu katika Hospitali ya Steve Biko mjini Pretoria nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa shambulizi la moyo.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW