DStv Inogilee!

Nicki Minaj amshushia onyo kali Cardi B ‘ukiendelea hivyo utauawa’

Rapper wa kike nchini Marekani, Nicki Minaj ameamua kumuonya mwenzake Cardi B kwa kumwambia kuwa endapo ataendelea na tabia zake za ukorofi kama alivyomfanyia yeye wikiendi iliyopita basi atauawa mapema.

Image result for NICKI MINAJ VS CARDI b
Nicki Minaj

Nicki amesema hayo kwenye show yake ya Queens Radio inayosikika kupitia Apple Music’s Beats 1 jana Jumatatu, kuwa tabia ya Cardi B ni mbaya na akiendelea kuwafanyia watu wengine basi atauwa.

Unakuwa mwepesi wa kunyanyua mikono yako juu na kurusha maneno makali mbele ya watu, nadhani ukiendelea hivyo kuna baadhi ya watu watakuua, Kumbuka hilo na huu ndio ukweli hakuna utani kama huo,“amesema Nicki Minaji na kumchimba kwa undani Cardi B.

Siajawahi kuwa malaya wacheza uchi ndani ya klabu (Strippers) au malaya wanaojionesha kwenye Reality Show, fedha zangu naingiza kwa jasho langu mwenye toka kitambo.“amemaliza Nicki Minaj.

Nicki na Cardi B walirushiana maneno na nusura wazichape sikubya Ijumaa kwenye maonesho ya fasheni ya Harper’s Bazaar jijini New York, Marekani.

Chanzo cha ugomvi wa wawili hao imeleezwa kuwa Nicki Minaj alibadili mashairi katika wimbo wa Motorsport wa Migos, ambapo ilidaiwa kuwa Nicki Minaj aliingiza mistari mwanzo halafu akafuata Cardi B. Lakini baadaye baada ya kurudi Nicki alipata wasaa wa kuisikiliza mistari ya Cardi B na yeye kugundua kuwa msanii huyo amemfunika hivyo Nicki aliomba kubadili mistari yake katika ngoma hiyo,hapo ndipo mwanzo wa Ugomvi ulipoanzia.

Hata hivyo, Nicki Minaj alishawahi kunukuliwa kwenye moja ya interview yake na Beatz  Radio, akisema kuwa Cardi B hampi heshima tangu washirikishwe wote kwenye ngoma ya Motorsport.

Cardi B naye amekuwa akimshutumu Nicki Minaj kuwa anasambaza habari za uongo kwenye vyombo vya habari jambo ambalo linamkera.

SOMA ZAIDI – Hiki ndio kilichopelekea Nicki Minaj na Cardi B kutaka kudundana kwenye sherehe za Harper’s Bazaar ICONS

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW