Burudani

Baada ya Madee kukosoa Bongo Flava, Nikki wa Pili ajibu mapigo

Rapper Niki wa Pili ameshindwa kuvumilia kauli ya Madee aliyoitoa kupitia mtandao wa Twitter.

Mapema Jumamosi hii, Madee kupitia mtandao huo alianzisha mjadala kuhusu muziki wa Bongo Fleva kukosa tuzo na albamu. Madee ameandika, “Mziki wetu umepata kilema! hauna TUZO hauna ALBUM halafu kuna watu wanasema wanataka kuufikisha mbele, hahah kwa njia gani labda ,”

Sasa msanii Nikki wa Pili ametoa maoni yake kuhusu kauli hiyo ya hitmaer huyo wa Hela, kwa kusema si kweli kwamba muziki amepata kilema kwani muziki unakuzwa na vipaji na sio tuzo wala albamu.

“Tuzo au albamu ni vitu vya kusogeza tu lakini pia albamu hazijatoka kutokana na matatizo ya kisoko lakini sio kama muziki wetu umepata kilema. Mimi naona muziki ndani ya talent za wasanii wenyewe as long as una kipaji kikali utakuwa na muziki mkali. Unaweza kuwa na tuzo na albamu lakini kama huna talent huwezi kuwa na muziki,” Nikki amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Hivyo vitu sivikatai vinasaidia muziki lakini muziki unaanza vipi? Je kuna watu wenye talent, maprodyuza wakali, kuna watu wenye uwezo wa kuimba na ku-deliver muziki mzuri, muziki utatusua,” ameongeza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents