Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Baada ya Manji kutua uraiani, Wema Sepetu aandika ujumbe huu

Baada ya mfanyabiashara, Yusuf Manji kuachiwa huru Mahakama ya Kisutu leo, Malkia wa Bongo movie,Wema Sepetu ameonyeshwa kufurahishwa mfanya biashara huyo kurudi uraiani.

Wema sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram ametumia ukurasa wake huo akiwa amempost mfanyabiashara huyo na kuandika “Alhamdulillah,”

Manji na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh. milioni 192.5 wameachiwa huru baada ya kesi yao kufutwa na Mahakama ya Kisutu.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW