Habari

Baada ya miaka 10; Shirika la Reli Tanzania laanza kusafirisha mizigo Uganda

Shirika la Reli Tanzania {TRC} limeanza kusafirisha mizigo kwenda Kampala nchini Uganda ikiwa ni miaka takribani 10 tangu usafiri wa mizigo kwenda Uganda kupitia reli usitishwe.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Treni hiyo huvuka ziwa Victoria kwa kutumia MV Umoja.

“Shirika la Reli Tanzania {TRC} laanza kusafirisha mizigo kwenda Kampala Uganda ikiwa ni miaka takribani 10 tangu usafiri wa mizigo kwenda Uganda kupitia reli usitishwe. Treni hii huvuka ziwa Victoria kwa kutumia MV Umoja.Hongera Serikali ya Awamu ya Tano,” ameandika Msigwa kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo Msigwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents