Michezo

Baada ya miaka 20, Arsenal watupwa nje ya ‘Top Four’ (+Video)

Klabu ya Arsenal jana imeshindwa kufuzu kwa kombe la klabu bingwa barani ulaya (Champions League) kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 licha ya ushindi mnono dhidi ya Everton wa mabao 3-1 katika siku ya mwisho ya mechi za ligi kuu England.

Arsenal ilianza mechi vizuri ikiwa na pointi moja nyuma ya Liverpool na walikuwa katika nafasi nzuri ya kuchukua nafasi yao ya nne waliyoizoea miaka yote wakati waliongoza mnamo dakika ya nane.

Lakini Mpaka kipenga cha mwisho kinalia Liverpool alikuwa tayari kashamtandika Middlesbrugh Goli 3-0 na kufanya hesabu za Arsene Wenger za kucheza Klabu bingwa zigonge mwamba.

Klabu ya Manchester City imeshika nafasi ya tatu na kufuzu moja kwa moja kucheza Klabu Bingwa baada ya kuinyuka Watfoird mabao 5-0.

Tazama Magoli ya Arsenal hapa chini.

https://youtu.be/Ri9PZS-HK5Y

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents