Burudani

Baada ya Mpe Habari kuna ‘msiba’ mwingine – Stereo

Rapper Stereo amechimba mkwara mzito kwa ujio wa ngoma yake mpya.

Baada ya ya kufanya vizuri na ngoma ‘Mpe Habari’ aliyomshirikisha Rich Mavoko, Stereo amesema kinachofuata ni kutoa remix ya ngoma hiyo kisha project mpya inafuata.

“Wiki hiyo inayokuja nitatoa remix ya Mpe Habari ambayo nimewashirikisha Stamina, Bill Nass, na baada ya hapo kuna msiba mwingine unakuja,” Stereo ameiambia Bamiza Top 20 ya Magic Fm.

Ngoma ya Mpe Habari ambayo ilitoka June 13 mwaka huu hadi sasa katika mtandao wa YouTube imepata views 949,586 kitu ambacho Stereo ameeleza kuwa ni mafanikio makubwa kwake kwani hakuna wimbo wake wowote uliofikia kiwango hicho cha views.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents