Baada ya Msemaji wa Serikali kusema Tanzania kinara wa utawala bora Afrika Mashariki , ACT Wazalendo wamjia juu (+Video)

Baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas kutoa taarifa ya Jarida la The Economist iliyoonyesha Tanzania ni kinara wa utawala bora Afrika Mashariki ,Chama cha ACT -Wazalendo wameibuka kutengua hoja hiyo kwa kudai kuwa ni upotoshaji na propaganda zake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya Chama hicho, Katibu Itikadi wa Chama hicho, Ndugu Ado Shaibu amesema kuwa Msemaji wa Serikali amekwepa kueleza maudhui yaliyoibuliwa na Chama hicho huku wakitoa mapendekezo yao.

Aidha chama hicho wamemtaka Msemaji huyo aache tabia ya kuchukua taarifa vipande vipande na kuziweka kwa umma, huku wakidai kuwa rekodi ya nchi kwenye masuala ya haki za binadamu duniani imeporomoka sana.

Hata hivyo walitoa mapendekezo yao ikiwa ni pamoja na (!) Kuitaka serikalu iondoe zuio batili la vyama vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi (2)wameitaka serikali itoe taarifa ya uchunguzi kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi,Azory Gwanda.

Februari 7 mwaka huu Msemaji wa Serikali akizungumza na wana habari alisema kuwa Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2, mwaka huu na kuchapishwa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika masuala ya Utawala Bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Tazama video hii akizungumza:

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW