Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Baada ya Peter Okoye, Kcee aichana serikali ya Nigeria

Baada ya msanii Peter Okoye kutoka kundi la P-Square kutoa kauli ya kutopendezwa na maamuzi ya serikali ya Nigeria kuhusu kuwazuia wasanii wa muziki na waigizaji kushoot video nje ya nchi hiyo, naye Kcee ameonesha kutofurahishwa na suala hilo.

Kupitia mahojiano aliyofanya na kituo cha runinga cha Wotzup ONTV, mkali huyo amesema kuwa serikali ya Nigeria ikiamua kufanya suala hilo wajue kabisa kuwa watasababisha kiwanda cha burudani cha nchi hiyo kushuka katika soko.

Msanii huyo ameongeza kuwa, itakuwa ngumu kumlazimisha msanii mwingine kufika nchini hapo kwa ajili ya kufanya video.

Uamuzi huo ulitolewa siku ya Jumamosi na Waziri wa Habari na Utamaduni wa nchi hiyo, Lai Mohamed wakati wa mkutano wake na Copyright Society of Nigeria (COSON) lengo ni kuhakikisha wanasaidia kukuza kiwanda cha burudani na uchumi wa nchi hiyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW