Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Baada ya Waziri Nchemba kuonya wanaopanga maandamano, Mh. Lema anena

By  | 

Baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuonya wanaotaka kufanya maandamano, Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa kauli aliyoitoa sio ya bahati mbaya.

Lema amemuhoji Waziri Nchemba akisema kuwa “unasema kuna watu wanapanga mauaji ili kuichafua taswira ya Nchi huku akisema kuwa maelekezo uliyo nayo ni kumbambikia Mh Mbowe kesi ya Mauaji”.

Mwigulu,kauli yako Singida sio ya bahati mbaya.Unasema kuna watu wanapanga mauaji ili kuichafua taswira ya Nchi, maelekezo uliyo nayo ni kumbambikia Mh Mbowe kesi ya Mauaji pamoja na Viongozi wengine, huu Mpango wenu mnaonekana bado mnao.Hivi Dr Kipilimba bado anahubiri Injili”? amehoji Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Waziri Nchemba jana alimuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote wanaopanga mipango ya kuandamana.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW