Burudani

Baada ya Willy Paul huyu ni msanii mwingine aliyezulu WCB

Baada ya staa wa gospel Willy Paul Msafi kutoka nchini Kenya anayetamba na ngoma I Do aliyomshirikisha mrembo kutoka Jamaica, Alaine kuzulu ofisi za WCB, sasa imekuwa ni zamu ya staa mwingine wa Kenya anayetokea mji wa zama wa pwani ya Kenya Mombasa kwa jina Chikuzee.

Chikuzee aka Zee la Mavuvuzela ni maarufu sana haswa ikizingatiwa style yake ya muziki anayotumia kuwa ya aina yake pamoja na sauti na mihemko inayodurusu kukamilisha burudani kamili kwenye fani ya muziki.

Mashabiki wake walifurahia punde tu Chikuzee alipokonyezea picha alizopiga kwenye ofisi za WCB huku nyingine akiwa na CEO wa kampuni hiyo ya muziki na staa wa kibao Marry you Diamond Platnumz.

Haijabainika wazi ni kwa madhumuni gani Chikuzee kuitembelea WCB, lakini tetesi zipo hewani kuwa kuna kitu kiko jikoni baina ya mkali huyo wa ngoma Si Vibaya na Raymond wa WCB. Huku wengine wakihoji kuwa huenda alifika pale ili kutia sahihi mkataba wa kuwezesha ngoma zake kuwekwa kwenye wavuti/tovoti ya kununua mziki ya wasafi.com.

Hata hivyo Diamond kuna kipindi alihojiwa kwenye kipindi cha Mambo Mseto kupitia redio Citizen ya nchini Kenya na alishawahi kukiri kuwa kati ya wasanii wa nchini Kenya anaowakubali na kuwaelewa zaidi na hangesita kufanya kazi nao nafasi ingetokea basi Chikuzee ni mmoja wao.

Hivyo si ajabu leo hii kuona kazi ya Diamond na Chikuzee. Diamond anazidi kuzivutia, kuzigusa na kuziongoa nyoyo za mashabiki wake haswa wa kanda ya pwani ya Kenya kwa kuonyesha kuwa anawakubali na yuko tayari kufanya kazi na wanamuziki wa ukanda huo pia bila kujali ukubwa alionao kwa sasa kimuziki duniani.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents