BurudaniUncategorized

Baada ya Z Anto kutoa ngoma moja, ‘nina ngoma zisizopungua 18’

Msanii wa Bongo Flava, Z Anton amesema licha ya kutoa ngoma moja katika ujio wake mpya kuna nyingine 18 zipo tayari.

Hitmaker huyo wa ngoma kama Binti Kiziwi na Mpenzi Jini ameeleza kuwa idadi hiyo ni katika awamu hii ya kwanza pekee na awamu nyingine itakuwa na ngoma zake.

“Kwa wakati huu naamini stoo yangu ina ngoma za kutosha, ngoma ambazo nimeziandaa kwa awamu hii ya kwanza ni ngoma zisizopungua 18 hivi ambazo nimeziweka” Z Anto ameiambia Bongo5.

“Tulikaa watu wengi kupendekeza kazi ipi itoke katika zile tatu za mwanzo katika zile 18 ipo ambayo ilipendekezwa tofauti na hii ‘Kacheze Unapochezaga’ licha ya kuwa kali sana lakini tukaona hii ni neno ambalo watu wanaweza kuikariri haraka” ameongeza.

Katika hatua ngingine amesema anajua kuwa kazi yake mpya kuna watu watachomwa na kuna watu wataumizwa na pengine kuna watu watatia nia ya kumtafuta ila anaomba wasifike huko kwani alichoimba ni ukweli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents