Habari

Baba aichoma moto familia yake na kujiua akiogopa deni la tsh 4,300/=

Baba mmoja katika mji wa Coimbatore nchini India ameiteketeza familia yake kwa kuichoma moto akikwepa kulipa deni la Shilingi 4,300/= za kitanzania.

Miili mitatu ya familia iliyoungua kwa moto ikipelekwa hospitali mapema jumatatu baada ya kutokea kwa tukio hilo

Mwanamme huyo aliyetambulika kwa jina la Esakimuthu alifanya tukio hilo siku ya jumatatu tarehe 23 Otoba ambapo aliwamwangia mafuta ya taa mke wake aliyetambulika kwa jina la Subbulakshmi na watoto wake wawili wakiwa wamelala na kuwachoma moto kisha na yeye kujiua .

Ndugu wa karibu wa Esakimuthu wanasema kijana huyo alikuwa na mikopo kwenye mabenki na madeni lukuki kutoka kwa marafiki zake.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo majirani waliipeleka hospitali familia hiyo lakini hawakufanikiwa kuokoa maisha yao.

Polisi mjini Coimbatore nchini India jana wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo mnamo tarehe 23 Oktoba mwaka huu na watu watatu wamefariki kwenye tukio hilo.

Taarifa za uchunguzi kutoka polisi zinasema mdaiwa huyo kabla ya kuchoma moto familia yake kuna mtu alikuja nyumbani kwake siku moja kabla ya tukio akimdai kiasi cha rupia 96  kama ongezeko baada ya kumkopesha rupia 1 miezi mitatu iliyopita.

Polisi wamekiri kuwa mdaiwa wiki iliyopita alitoa taarifa kwao kutaka suala la kudaiwa lisuluhishwe, hata hivyo polisi walimtaka alipe kiasi hicho kama walivyokubaliana ndipo mdaiwa akachukua uamuzi huo.

Chanzo:The Hindu

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents