Habari

Baba ampa mimba mama na binti yake, Watokomea kusikojulikana, Mama aeleza ilivyokuwa – Video

Baba ampa mimba mama na binti yake, Watokomea kusikojulikana, Mama aeleza ilivyokuwa - Video

Deus Richard 40, mkazi wa Kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amempa ujauzito binti yake wa Darasa la Nne, Monika Shigela, na kumtelekeza mkewe na watoto wadogo watano na kutoweka kusikojulika na mtoto wake aliyempa mimba.

Bi Mariam Masanja ambaye ndiye Mke aliyetelekezwa, amesema kuwa alipobaini uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanae na Baba yake aliwaeleza viongozi wa Dini, kitendo ambacho kilimkasilisha bwana huyo na kuanza kuonesha bayana mapenzi yake na mtoto wake.

Aidha Mariam ameongeza kuwa licha ya ugumu wa maisha anaopitia kwa sasa, kutokana na kutelekezwa akiwa na watoto wadogo na pia ndani kukiwa hakuna chakula, anaiomba Serikali kumkamata mumewe na kumchukulia hatua kali za kisheria.

https://www.instagram.com/p/B7bEH7tB3vv/

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents