Burudani

Baba Harmorapa afunguka kuhusu ndugu ‘feki’ aliyedai ana undugu na Harmorapa

Baada ya kijana aliyedai kusafiri kutoka Iringa kuja Dar es salaam kwaajili ya kumtafuta Harmorapa kwa madai ni ndugu yake na baadaye Harmorapa kumkataa, Baba wa Harmorapa amempigia simu mwanaye na kumuondoa shaka kuhusu kijana huyo.

Harmorapa akiwa na kijana huyo

Kijana huyo aitwae Frank Omary amedai aliamua kumtafuta Harmorapa baada ya mama yake kumwambia kwamba  rapa huyo ni ndugu yake ambaye wamechangia baba..

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Harmorapa amedai baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo mtandaoni alipigiwa simu na baba yake mzazi.

“Nimetoka kuongea na baba yangu amesema siyo kweli, huyo mtu hamfahamu kabisa,” alisema Harmorapa ambaye yeye ni mtoto wa pili kwa upande wa baba yake. “Baba mwenyewe amemshangaa sana, hata jina la huyo jamaa halijui ndio maana akaniambia kwamba huyo sio ndugu yako,”

Harmorapa amemtaka kijana huyo kutafuta ishu nyingine ya kufanya na kuacha kupoteza muda katika mambo ambayo amedai hayawezi kumsaidia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents