Burudani ya Michezo Live

Baba Levo ameshinda rufaa yake, Zitto athibitisha

Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhe. Clyaton Revocatus Chipando (Baba Levo) leo ameshinda Rufaa yake katika Mahakama ya kuu Mkoa wa Kigoma.

Awali alihukumiwa kifungo cha miezi 6 katika mahakama ya Mwanzo mwandiga alipokata Rufaa katika mahakama ya Mkoa akahukumiwa kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 jela na leo ameshinda ktk Rufaa yake mahakama kuu.

Baba levo alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani.

Leo Mh Jaji amefuta hukumu ya mahakama ya wilaya na Baba levo yupo huru kutokana kifungo chake kilikua kinaishia tarehe 11/11/2019 siku ya jumanne na sasa Baba levo yupo huru.

Tunashukuru maamuzi ya mahakama kuu haki imetendeka na sio haki kutendeka tu haki imeonekana imetendeka.

Baba levo ni mtetezi wa Bodaboda,Bajaji na wanyonge wajasiliamali katika manispaa amewapambania vya kutosha leo ametoka Usichoke kuwatetea wananchi wa mji mzima ndio alivyozaliwa baba levo hii ndio safari ya kuwa mwanasiasa mkubwa nchini.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW