Bongo Movie

Baba Lulu aomba kesi ya mwanaye iachiwe mahakama

Baba mzazi wa malkia wa filamu, Elizabeth Michael, Mzee Michael Kimemeta, amefunguka juu ya matatizo yanayomkabili binti yake.

Lulu akiwa Mahakama Kuu siku ya jana

Mzee Michael ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa tukio la kifo cha Kanumba lilitokea wakati mrembo huyo akiwa na umri mdogo, na kuwataka watu kutohukumu na kuviachia vyombo husika vifanye uamuzi wake.

Katika hatua nyingine, mzee huyo alisema kwamba huenda malezi ambayo alikuwa anayapata na kumuacha huru zaidi kufanya akipendacho, ndio kilichomsababishia mwanaye kukutwa na maswahibu hayo.

“Kuja kwenye tasnia yake sikuona ajabu pamoja na kwamba sikujua kama angekuja kwenye tasnia hii ya usanii, tungekuwa kama wazungu kuangalia watoto ningegundua mapema, maana dalili zilikuwa zinaonekana tangu zamani, ndio maana nilikuwa namkazania kusoma na siku-‘favour’ sana mambo yake ya sanaa ”, alisema mzee Kimemeta.

Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents