Burudani

Baba mzazi wa Beyonce athibitisha kupata wajukuu mapacha

Baada ya kusambaa kwa tetesi za Beyonce na Jay Z kupata mapacha wao – Baba mzazi wa Queen Bey ambaye pia aliwahi kuwa meneja wake, Mathew Knowles amethibitisha hilo.

Jumapili hii mzee Knowles aliweka picha hiyo hapo chini ya kadi kwenye mtandao wa Twitter akipongeza kuzaliwa kwa mapacha hao na kuandika, “They’re here! #beyonce #twins #jayz #happybirthday.”

Katika kuthibitisha jambo hilo ni kweli, mzee Knowles aliweka picha hiyo hiyo kwenye mtandao wa Instagram na mama yake Beyonce aliweza ku-like picha hiyo.

Kwa mujibu wa TMZ, inadai kuwa watoto hao wamezaliwa Jumatatu iliyopita ya Juni 12 lakini mpaka sasa bado wapo hospitalini hawajaruhusiwa wakiwa chini ya uangalizi pamoja na mama yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents